Kadi za Kidijitali Tanzania
Kadi ya kidijitali ni kadi ya mialiko inayotumwa kwa link — WhatsApp au SMS — badala ya karatasi. Kila mgeni anapata toleo lake lenye jina lake, anaweza kujibu, kuona meza yake, na kuonyesha QR mlangoni. KadiX inatengeneza kadi hizi kwa harusi, send off, mahafali, michango na matukio ya kampuni Tanzania.
Mifano ya kadi za kidijitali
Kila kadi inaonekana vizuri kwenye simu — ndio mahali wageni wengi wataifungua.
Harusi — Minimal (Sage & Blush)
Send-Off — Boarding Pass
Graduation — Modern Badge
Corporate — Geo Grid
Birthday — Glossy Gradient
Kumbukumbu — Laurel Wreath
Engagement — Ring Emblem
Kitchen Party — Kanga (Indigo)
210+ miundo iliyotengenezwa tayari. Ukichagua moja, tunaibadilisha rangi, picha na maneno kwa tukio lako.
Kadi ya kidijitali ni nini?
Kadi ya kidijitali ni toleo la kidijitali la kadi ya mialiko. Badala ya kuchapisha na kusambaza kwa mkono, mgeni anapokea ujumbe wenye link; link inampeleka kwenye kadi yake mwenyewe yenye jina lake. Kwa kuwa ni ukurasa, kadi inaweza kufanya mambo ambayo karatasi haiwezi: kujibu RSVP, kuonyesha meza, kufungua ramani, na kutoa QR ya kuhakiki mlangoni.
Kwa mgeni, inaonekana kama kadi nzuri tu. Kwa mwenye sherehe, ni mfumo mzima wa kufuatilia wageni.
Tofauti kati ya kadi ya kidijitali na kadi ya karatasi
| Kadi ya kidijitali | Kadi ya karatasi | |
|---|---|---|
| Gharama kwa mgeni | TSh 1,000–1,500 | Print, bahasha na usafirishaji |
| Jina la kila mgeni | Ndiyo | Kwa kuandika mkono au print tofauti |
| Usambazaji | WhatsApp na SMS, sekunde chache | Kwa mkono, siku kadhaa |
| RSVP | Mgeni anajibu mwenyewe | Simu au ujumbe kwa mwenye sherehe |
| Meza na QR | Zinaonekana kwenye kadi | Hapana |
| Mabadiliko | Bila kuchapisha tena | Chapisha upya |
Kwa nini kadi za kidijitali zinatumika Tanzania?
Kwa sababu WhatsApp ndio mahali watu wanapotumia muda wao, na SMS inafika hata kwenye simu za kitochi. Kadi ya kidijitali inaondoa gharama ya print, usafirishaji na kufuatilia wageni kwa daftari. Mgeni hawezi kudai hakupata mialiko — ujumbe uko kwenye simu yake, na mwenye sherehe anaona ni nani amejibu na ni nani hajajibu.
Kwa matukio ya kampuni, kadi hiyo hiyo inaweza kuwa usajili wa washiriki: mshiriki anajisajili mwenyewe, anapata pass yenye QR, na mlangoni anahakikiwa.
Digital invitation cards in Tanzania
KadiX builds personalised digital invitation cards for events across Tanzania. Each guest receives their own card by WhatsApp or SMS, with the event details, their table, RSVP and a QR code for door check-in. Cards are designed in Swahili or English, and can be printed from a downloadable image when paper copies are needed.
Kadi za kidijitali kwa kila aina ya tukio
- Kadi za harusi — ikiwemo nikkah na mitindo ya simu (9:16).
- Kadi za send off — pamoja na ufadhili na michango.
- Kadi za mahafali — shule, chuo na chekechea.
- Kadi za mchango — kila mchangiaji na kadi yake.
- Kadi za mialiko — kitchen party, birthday, aqiqah, baby shower na kumbukumbu.
- Matukio ya kampuni — mikutano, kongamano, uzinduzi na usajili wa washiriki.
Usalama na faragha
Kila kadi ina link yake ya siri yenye mchanganyiko wa herufi na namba — hakuna namba ya mgeni inayoonekana kwenye link. Mtu asiye na link hawezi kufikia kadi. Kadi ya mgeni mmoja haionyeshi orodha ya wageni wengine wala taarifa zao.
Bei ya kadi za kidijitali
TSh 1,000 kwa kadi ya kawaida na TSh 1,500 kwa muundo wa premium. Usajili wa washiriki ni TSh 1,000 kwa mshiriki. Sampuli unaiona kabla ya kutuma.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kadi za kidijitali ni nini?
Kadi ya kidijitali ni kadi ya mialiko inayotumwa kwa link (WhatsApp au SMS) badala ya karatasi. Ina jina la mgeni, maelezo ya tukio, meza na QR ya check-in.
Kadi za kidijitali zinatofautiana vipi na PDF?
PDF ni picha tuli. Kadi ya kidijitali ni ukurasa: mgeni anajibu RSVP, anaona meza, anafungua ramani, na QR yake inatumika mlangoni. Unaweza bado kupakua picha ya kadi na kuchapisha.
Mgeni asiye na smartphone atapataje kadi?
Anapokea SMS yenye jina lake na code ya mialiko. Mlangoni, staff anaingiza code hiyo kwenye mfumo na mgeni anahakikiwa.
Je, kadi zinafanya kazi bila internet?
Kufungua kadi kunahitaji internet, kwa hivyo tunatoa pia picha ya kadi (JPEG) ya kuchapisha, na SMS yenye code kwa wasio na smartphone.
Kadi za kidijitali zinagharimu kiasi gani Tanzania?
TSh 1,000 kwa kadi ya kawaida na TSh 1,500 kwa premium. Usajili wa washiriki ni TSh 1,000 kwa mshiriki.