Kadi za mialiko · Michango · QR check-in

Zaidi ya mialiko.

Tuma tu orodha ya wageni, iwe kwenye karatasi au Excel. Tunatengeneza kadi nzuri, kila mgeni anapokea yake kwa WhatsApp au SMS (hata mwenye simu ndogo), na siku ya sherehe tunahakiki wageni mlangoni kwa QR.

  • Kazi inaanza ndani ya saa 24
  • Unaona sample kabla ya kutuma
  • Kuanzia TSh 1,000 kwa kadi
210+Miundo ya kadi
20Aina za matukio
24hTunaanza kazi ndani ya saa 24
SMSHata simu ndogo inapata kadi
Rahisi kwa hatua 4

Wewe tuma orodha. Mengine tunafanya sisi.

1

Tuma orodha

Majina na namba za simu: picha ya karatasi, Excel au ujumbe wa WhatsApp. Tunaipanga sisi.

2

Chagua muundo

Zaidi ya miundo 210, ya picha au ya rangi. Tunakutumia sample uthibitishe kwanza.

3

Tunatuma kadi

Kila mgeni anapata kadi yenye jina lake na QR yake kwa WhatsApp au SMS. Unaona nani amepokea na nani amethibitisha.

4

Siku ya sherehe

QR inasomwa mlangoni kwa sekunde mbili. Kadi moja haitumiki mara mbili, na wasioalikwa hawapiti.

Au fanya mwenyewe

Tengeneza kadi zako mwenyewe, kwa simu yako.

Fungua akaunti, weka tukio na wageni wako, kisha tuma kadi wewe mwenyewe. Kufungua akaunti ni bure.

  1. 1
    Fungua akaunti

    Jina, namba ya simu na nenosiri. Utapokea namba ya uthibitisho kwa SMS.

  2. 2
    Weka tukio na wageni

    Andika taarifa za sherehe, kisha ongeza wageni mmoja mmoja au kwa faili la Excel.

  3. 3
    Chagua muundo

    Ona kadi yako bure kabla ya kulipia, na weka picha yako ukipenda.

  4. 4
    Tuma kwa wageni

    Kila mgeni anapata kadi yake kwa SMS au WhatsApp, yenye QR ya mlangoni.

Miundo

Kadi nzuri kwa kila aina ya sherehe.

Hizi ni kadi halisi kutoka kwenye mfumo wetu, kati ya miundo zaidi ya 210. Kila mgeni anapata yake, yenye jina lake na QR yake.

Harusi Kitchen Party Kuposana / Uchumba Send-Off Baby Shower Aqiqah Siku ya Kuzaliwa Mahafali Maadhimisho ya Ndoa Kampuni Mkutano Ibada / Tukio la Kidini Komunyo ya Kwanza Party Tuzo Kumbukumbu Harambee Uzinduzi wa Bidhaa Michezo Nyingine

Unaweza kuweka picha zenu, nembo au rangi za sherehe yako.

Huduma

Kila kitu cha tukio lako, mahali pamoja.

Kadi za mialiko

Harusi, send-off, kitchen party, birthday, kumbukumbu na sherehe zote.

  • Kadi binafsi: jina la mgeni na QR yake
  • WhatsApp na SMS, hata simu ndogo
  • RSVP: mgeni anathibitisha kufika
  • Ukurasa wa mgeni: ramani, ratiba na picha
  • Ukumbusho kabla ya siku ya tukio

Michango

Kamati za harusi, misiba, harambee na vikundi.

  • Kadi na link binafsi ya kila mchangiaji
  • Ahadi, kilicholipwa na salio papo hapo
  • Vikumbusho kwa SMS hadi siku ya tukio
  • Malipo kwa simu na SMS ya shukrani
  • Akaunti ya mweka hazina na katibu

Usajili na taasisi

Mikutano, makampuni, shule, makanisa na SACCOS.

  • Link moja ya usajili kwa washiriki wote
  • Pass ya kidijitali yenye QR
  • Uuzaji wa tiketi kwa pesa ya simu
  • Orodha, ripoti na check-in mlangoni
  • Mikataba ya muhula au mwaka
Huduma kwa mteja

Hauko peke yako. Tuko nawe hadi mgeni wa mwisho aingie.

Huduma kwa mteja ndiyo msingi wa KadiX. Una mtu halisi wa kuwasiliana naye kila hatua, kwa WhatsApp au simu.

Tunaanza ndani ya saa 24

Ukishatuma orodha na kuthibitisha, kazi inaanza siku hiyo hiyo.

Unaona kabla ya kutuma

Tunakutumia sample ya kadi uthibitishe majina, tarehe na muundo.

Timu yetu mlangoni

Tunaweza kuleta timu ya QR check-in siku ya sherehe yako.

Taarifa zako ni siri

Namba za wageni wako tunazitumia kwa tukio lako tu, hatuzishiriki na mtu mwingine.

Matukio yetu

Sherehe tulizosimamia

Takwimu halisi za siku yenyewe, na maneno ya wateja wetu baada ya tukio.

★★★★★

“kadix mko vizuri sana nimewatafuta siku 2 kabla na mialiko imewafikia watu wote”

The Wedding Celebration
Dotto
Dotto Bwana harusi
Bei

Bei wazi, bila gharama zilizojificha.

Unalipia kwa kila mgeni tu. Bei hizi ni za kuanzia, na tunazirekebisha kulingana na ukubwa na mahitaji ya tukio lako.

Kadi Standard

TSh1,000kwa kadi
  • Kadi ya kidijitali iliyosanifiwa
  • Inatumwa kwa SMS na WhatsApp
  • Ukumbusho kabla ya tukio
Wageni 200 = TSh 200,000

Michango Standard

TSh 1,000kwa mchangiaji

Kadi ya mchango, kurekodi ahadi, ukumbusho mara 3 na ripoti kwa kamati.

Michango Pro

TSh 1,500kwa mchangiaji

Link binafsi (ahadi, kilicholipwa, salio), ukumbusho kila wiki, malipo kwa simu na SMS ya shukrani.

Usajili & Guest Pass

TSh 1,000kwa mshiriki

Link moja ya usajili, pass yenye QR, orodha na check-in.

Shule, makanisa, SACCOS, makampuni

Kuanzia TSh 500kwa mwanachama, kwa muhula

Mkataba wa muhula au mwaka. Tunaandaa nukuu ya tender.

Mialiko + Michango = punguzo 10%

Mfano: kadi 200 (200,000) + Michango Pro 150 (225,000) = 425,000. Unalipa TSh 382,500.

Huduma za ziada

Timu ya QR check-in mlangoniTSh 50,000 / tukio
Simu za mwaliko kwa wageni maalumBURE
Kiwango cha chini cha kaziTSh 50,000

Malipo: 50% kuanza kazi, salio kabla ya tukio · M-Pesa, Tigo Pesa au benki.

Maswali

Maswali yanayoulizwa mara nyingi.

Wageni wangu wanapokea kadi vipi?

Kila mgeni anapokea kadi yake binafsi kwa WhatsApp au SMS: link inayofungua kadi yenye jina lake na QR yake ya kuingia.

Mgeni hana WhatsApp au ana simu ndogo?

Hakuna shida. Anapokea mwaliko wake kwa SMS ya kawaida, yenye maelezo yote muhimu ya sherehe.

Orodha yangu iko kwenye karatasi. Inafaa?

Ndiyo. Piga picha ya karatasi na utume kwa WhatsApp. Tunaiandika na kuipanga vizuri sisi, kisha tunakutumia uithibitishe.

Naweza kuweka picha zetu au nembo kwenye kadi?

Ndiyo. Miundo mingi inakubali picha za maharusi, mwenyeji au nembo ya tukio, na tunaweza kutumia rangi za sherehe yako.

Bei inapangwaje?

Unalipia kwa kila mgeni, kuanzia TSh 1,000 kwa kadi. Bei inarekebishwa kulingana na idadi ya wageni na huduma unazochagua. Unalipa 50% kuanza kazi na salio kabla ya tukio.

Michango inafanyaje kazi?

Kila mchangiaji anapata kadi na link yake inayoonyesha ahadi, kilicholipwa na salio. Vikumbusho vinaenda kwa SMS, na mweka hazina na katibu wanaona ripoti papo hapo.

Mnafanya usajili wa mikutano na taasisi?

Ndiyo. Tunakupa link moja ya usajili, kila mshiriki anapata pass yenye QR, na tunahakiki mlangoni. Kwa shule, makanisa na SACCOS tuna mikataba ya muhula au mwaka.

Taarifa za wageni wangu ziko salama?

Ndiyo. Majina na namba za wageni wako tunazitumia kwa tukio lako tu, na hatuzishiriki na mtu mwingine.

Naweza kutengeneza kadi mwenyewe?

Ndiyo. Fungua akaunti, tengeneza tukio, chagua muundo na uwatumie wageni wako mwenyewe kwa SMS au WhatsApp. Lakini wateja wengi hupendelea tuwafanyie kila kitu — tuma tu orodha yako.

Fungua akaunti →

Anza tukio lako

Tuambie kuhusu tukio lako.

Jaza fomu hii kwa dakika moja. Tutakupigia au kukutumia WhatsApp, na kukupa bei na sample.

Nini kinafuata

  1. Tunakupigia kuthibitisha mahitaji yako
  2. Unatuma orodha ya wageni
  3. Unapokea sample na bei kamili
Huduma unazohitaji

Tunatumia namba yako kukujibu tu. Hatutumi matangazo.

Ongea nasi